Thursday, 7 September 2017

Mwanasiasa wa upinzani Tanzania Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana

Mwanasiasa wa upinzani Tanzania Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana



Haki miliki ya pichaBUNGE
Image captionTundu Lissu,mwanasheria mkuu wa CHADEMA

Mwanasiasa wa upinzani nchni Tanzania Tundu Lissu ameripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania.
Mwanasiasa huyo amekimbizwa hospitali ya mkoa wa Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo limetokea wakati mbunge huyo akiwa nyumbani kwake.
Chama hicho kimelaani vikali tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi , Jires Mroto ameiambia BBC kuwa wameanza uchunguzi wa tukio hilo.
"Tunaomba wananchi wenye taarifa ya uhalifu huu, waweze kujitokeza" amesema Kamanda Mroto.
Hivi karibuni, mbunge huyo kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA, amekuwa akikamatwa mara kwa mara na polisi akishutumiwa kufanya uchochezi.
Akithibitisha tukio hilo,kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema " yupo hospitali, bado anajaribu kupambana kuokoa maisha yake"
Gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, limemnukuu Mganga mkuu wa hospitali ya Dodoma akisema wakili huyo ana majeraha ya risasi miguuni na tumboni.
Maelezo zaidi kufuata.

No comments:

Post a Comment

Watoto bado wanafanya kazi migodini, shambani’

Watoto bado wanafanya kazi migodini, shambani’   0 By Elizabeth Edward, Mwananchi eedward@mwananchi.co.tz Da...