Korea Kaskazini: Tutailetea Marekani machungu makubwa
Korea Kaskazini
imetishia Marekani na kusema kuwa itasababisaha machungu makali ambayo
Marekani haijawai kushuhudia kufuatia vikwazo vipya vilivyowekwa na
Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa Korea Kaskazini katika Umoja wa
Mataifa ameishutumu Marekani kwa kutafuta makabiliano ya kisiasa ,
kiuchumi na kijeshi.- Korea Kaskazini yasifia jaribio jingine la nyuklia
- Korea Kusini yafanya majaribio ya makombora kujibu majaribio ya Korea Kaskazini
Hatua hizo zinapiga marufuku uuzaji mafuta kwenda Korea Kaskazini na uuzuaji wa bidha kutoka Korea Kaskazini baada ya jaribio la sita na kubwa zaidi la bomu la nyuklia mapema mwezi huu.
Han Tae Song, ambaye ni balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa alisema amekataa kile alichokitaja kuwa vikwazo vilivyo kinyume na sheria.
"Hatua zitazochukuliwa na Korea Kaskazini zitaisababishia Marekani machungu makali ambayo hajawai kushuhudiwa katika historia yake," aliambia mkutano huko Geneva.
No comments:
Post a Comment