Saturday, 23 September 2017

Iran yafanyia majaribio kombora lake

Iran yafanyia majaribio kombora lake

  • 23 Septemba 2017


Image captionIran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.

Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.
Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa.
Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000.
Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo.
Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo.



Image captionRais Donald Trump na rais Rouhani wa Iran

Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea.

Tuesday, 12 September 2017

Chadema yawashukuru wote waliomchangia Lissu


CAHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewashukuru watu wote ambao wametoa michango yao kusaidia matibabu ya Tundu Lissu ambapo mpaka sasa zimepatikana Sh milioni 19.4. Kimesema hali ya mwanasheria wake huyo ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea kuimarika taratibu.
Akielezea hali yake kwa masikitiko leo, Katibu Mkuu wa Chadema, Vicent Mashinji amesema hali yake juzi mchana ilikuwa mbaya ambapo ililazimu kumsaidia kupumua kwa kutumia mashine lakini baadaye hali yake iliimarika.
"Hiyo ndio hali ya Lissu, jana hali ikua mbaya ikabidi awekewe mashine ya kupumulia lakini mchana hali ikaimarika wakatoa mashine na asubuhi leo ameamka vizuri anaendelea kupigania pumzi yake," amesema Mashinji.
Mashinji amesema jana saa nne asubuhi alianza kupata matatizo ya kifua ambayo pengine yalitokana na kulala muda mrefu. Mashinji amesema mpaka jana ambayo ni siku ya tano tayari Lissu ameshafanyiwa zaidi ya upasuaji tatu na kwamba imebidi kusitisha upasuaji ili mwili upumzike.
Amesema kwa sasa matibabu yanayoendelea kwa Lissu ni sehemu za ndani ya mwili ambazo zingehatarisha afya yake na kwamba sasa wataanza kushughulikia viungo vya nje. Chama hicho kimewashukuru watu wote ambao wametoa michango yao kusaidia matibabu ya Lissu ambapo mpaka sasa zimepatikana Sh milioni 19.4.



Watu nane wanasadikiwa kuvamia na kuvunja jengo la Prime House lililopo mtaa wa Tambaza eneo la Upanga karibu na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) usiku wabkuamkia leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amrthibitisha kuvamiwa na kuvunjwa kwa jengo hilo lenye ofisi mbalimbali ikiwamo ofisi ya Mawakili wa Prime Lawyers. Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mawakili wa Prime Lawyers amedai kwamba mlinzi wa jengo hilo amekutwa amefungwa kamba miguuni na mikononi pamoja na mdomo kwa kutumia plasta.
"Kwa sasa ni mapema sana kujua ofisi gani zilizoathirika kwenye uvamizi uliotokea, polisi wanaendelea na uchunguz kujua nini kilichotokea," ameeleza wakili huyo. Akizunhumza kwa njia ya simu asubuhi, Kamanda Hamduni amesema Polisibwako eneo la tukio kwa uchunguzi wa awali ili kujua ofisi zilizoathirika kutokana na tukio hilona kusudio la wavamizi hao.

Rais Magufuli amfariji Meja Jen. Mribata Lugalo

RAIS Dk John Pombe Magufuli amemtembelea Meja Jen. Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa katika hospitali ya Lugalo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio katika Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Meja Jenerali Mribata alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 na kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu. Mkuu wa Kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Rais kuwa mgonjwa anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi zilizokuwa mwilini katika sehemu za mkononi, kiunoni na tumboni.
Rais Magufuli ambaye aliambatana na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo ametembelea pia wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa waliokuwa katika wodi hiyo.
Rais Magufuli amewapongeza madaktari wa hospitali ya jeshi ya Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi kwa ujumla. Rais Magufuli amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono kwa kufanyia kazi changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Korea Kaskazini: Tutailetea Marekani machungu makubwa

Korea Kaskazini: Tutailetea Marekani machungu makubwa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Korea Kaskazini inasema imeunda na kulifanyia majaribio bomu la haidrojeni
Korea Kaskazini imetishia Marekani na kusema kuwa itasababisaha machungu makali ambayo Marekani haijawai kushuhudia kufuatia vikwazo vipya vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa ameishutumu Marekani kwa kutafuta makabiliano ya kisiasa , kiuchumi na kijeshi.
Mapema Marekani iliapa kuweka shinikizo zaidi ikiwa Korea Kaskazini itaendela na njia zake hatari.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Korea Kaskazini imekuwa ikifanyia majaribio makombora yake
Vikwazo vya Umoja wa Mataifa ni hatua ya kuhakikisha kuwepo uhaba wa mafuta na kipato kufuatia mipango yake ya nyulia.
Hatua hizo zinapiga marufuku uuzaji mafuta kwenda Korea Kaskazini na uuzuaji wa bidha kutoka Korea Kaskazini baada ya jaribio la sita na kubwa zaidi la bomu la nyuklia mapema mwezi huu.
Han Tae Song, ambaye ni balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa alisema amekataa kile alichokitaja kuwa vikwazo vilivyo kinyume na sheria.
"Hatua zitazochukuliwa na Korea Kaskazini zitaisababishia Marekani machungu makali ambayo hajawai kushuhudiwa katika historia yake," aliambia mkutano huko Geneva.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Umoja wa Mataifa umeiwekea vikwazo mara kwa 

Saturday, 9 September 2017

RAISI MAGUFURI AKIZA MARA MOJA WALIO MPIGA RISASI LISSU KUKAMATWA

h. Spika wewe pambana nao Bungeni nami nitawashughulikia nje ya Bunge. ~JOHN POMBE MAGUFULI
BAADA YA KUPIGWA RISASI MH. LISSU, ANAANDIKA KATIKA TWEETER YAKE.
Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka.
Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria. ~JOHN POMBE MAGUFULI.

RAISI WA KENYA UHURU KENYATA ATAKA ULINZI UIMALISHWE

Rais Uhuru #Kenyatta ameagiza ulinzi uimarishwe katk hospitali ya Agha Khan, Nairobi aliyolazwa Mhe.Tundu #Lissu.
-Tutumie fursa hii kumshukuru kwa kuona umuhimu wa kumlinda mpigania haki wetu.
Mungu ambariki sana.!

DEREVA WA TINDU LISSU

Shuhuda mmoja kutoka mkoani Dodma ameeleza kuwa Nyumba ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyepigwa risasi katika eneo la Area D Dodoma akiingia nyumbani kwake ipo karibu na nyumba ya naibu Spika wa bunge Dk Tulia Ackson Mwansasu.Amesema, ''nyumba ya naibu Spika huwa na Ulinzi mkali sana na askari wanaolinda hapo huwa na silaha nzito, ila sijafahamu kama siku hiyo ilikuwaje'' amesema.Dereva wa Tundu Lissu ambaye alishuhudia tukio hilo kwa karibu ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa, hawezi kuongea kwa sasa kwakuwa hayuko sawa.
Iwapo angepatikana dereva huyo, pia angeweza kuelezea mazingira ya tukio lenyewe, iwapo kulikuwa na walinzi katika eneo hilo ambalo nyumba ya Lissu ipo jirani kabisa na ile ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, yenye askari wenye silaha nzito.
Dereva huyo angeweza kujibu maswali wanayojiuliza wengi iwapo kama anaweza kuwatambua wahusika wa tukio hilo, ambalo katika moja ya maelezo yake, alidai kuwa aliliona gari jeupe aina ya Nissan iliyokuwa ikiwafuatilia ambalo watu hao waliomjeruhi Lissu walikuwa ndani yake.
CHANZO: Gazeti la Mtanzania

MWANAHARAKATI TINDU LISSU


KAULI YA TUNDU LISSU KABLA YA KUPIGWA RISASI


MBUNGE TUNDU LISSU ANUSURIKA KIFO



Thursday, 7 September 2017

USUPH MANJI ATUMBULIWA UDIWANI

YUSUPH MANJI ATUMBULIWA UDIWANI

SeeBait

Mfanyabiashara Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.


Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema hayo leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari.


Kutokana na hilo wamemuondoa Manji kwenye nafasi hiyo kutokana na kukosa sifa

UHURU KENYATTA AWAKATAA MAAFISA WAPYA WA TUME YA UCHAGUZI KENYA

UHURU KENYATTA AWAKATAA MAAFISA WAPYA WA TUME YA UCHAGUZI KENYA

SeeBait
Chama cha Jubilee cha Rais Uhuru Kenyatta kimewakataa maofisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya wa Urais mwezi ujao Oktoba 17,2017.


Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maofisa hao, ambao kimesema wanawafahamu kuwa wanapendelea wapinzani.


Siku moja iliyopita Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza maofisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika Oktoba 17 ambapo miongoni mwa maofisa hao ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na msimamizi wa kituo cha Taifa cha kujumlishia matokeo.


Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limesema "Tuna habari za kuaminika kwamba kwenye orodha ya maofisa hao kuna watu wanaofahamika wazi kuegemea upande fulani."


Leo Rais Uhuru amekutana na viongozi wa kidini ikulu ambapo amesema tarehe iliyotangazwa inafaa ili kutovuruga kalenda ya mitihani ya taifa ambayo imepangiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Oktoba.


Mahakama ya Juu nchini Kenya Septemba Mosi ilifuta matokeo ya Urais kwa kudai ulikuwa na dosari ambapo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8 ambao Rais Kenyatta alitangazwa mshindi.


Katika uchaguzi wa Agosti 8, Kenyatta alitangazwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27, huku mpinzani wake Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.


Hivi karibuni Muungano wa National Super Alliance (NASA), ambao mgombea wake ni Raila Odinga, ulidai mabadiliko makubwa kwenye IEBC kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.

WAZIRI SIMBACHAWENE AJIUZULU KWA AGIZO LA RAIS MAGUFULI SAKATA LA TANZANITE NA ALMASI

SeeBait
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti za uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi iliyoonyesha namna serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali.


Waziri Simbachawene ameandika barua hiyo muda mfupi tu tangu Rais Magufuli alipowataka viongozi wote aliowateua na wametajwa katika ripoti hiyo wakae pembeni ili kupisha uchunguzi ambao utakuwa huru na wa haki.


Mbali na Simbachawene, wengine waliokuwa wametakiwa kukaa pembeni ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani ambaye alituhumiwa kutotekeleza majukumu yake kikamilifu alipokuwa akifanya kazi katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lenye dhamana ya kusimamia madini.


Mbali na Ngonyani, mwingine ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi naye amepaswa kupisha uchunguzi ambao Rais ameagiza ufanywe na vyombo vya ulinzi na usalama haraka iwezekanavyo.


Rais Dkt Magufuli ametoa maagizo hayo leo alipokuwa akipokea ripoti hiyo ya uchunguzi wa madini kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliipokea jana kutoka katika kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.


Akiyasema hayo, Rais Magufuli aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi kwa wateule wake waliotajwa tajwa katika ripoti hizo lakini akasema kuwa, uchunguzi hauwezi kufanyika wakati kiongozi akiwa bado yupo serikali. Baada ya kusema hivyo, Rais Magufuli alisema anaamini kuwa viongozi hao watakaa pembeni kupisha uchunguzi.


Hafla hiyo ya kukabidhi ripoti ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Wenyeviti wa kamati mbili za Tanzanite na Almasi, Dotto Biteko na Mussa Azzan Zungu ambao wote ni wabunge.


Wengine waliohudhuria ni pamoja na viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na viongozi waandamizi wa serikali.


Rais Magufuli ameendelea kuwasisitiza watanzania kuwa wazalendo kwani rasilimali za nchini za nchi zinaibiwa na watanzania wanazidi kubaki katika umasikini uliokithiri.


Baada ya kuhutubia, Rais Magufuli alikabidhia nakala za ripoti hiyo kwa viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama ili vianze kufanya kazi mara moja na sio kuendelea kukaa huku mali za watanzania zikiibiwa.

Watoto bado wanafanya kazi migodini, shambani’

Watoto bado wanafanya kazi migodini, shambani’   0 By Elizabeth Edward, Mwananchi eedward@mwananchi.co.tz Da...